Hivi ama vile
Rostam (Roma & Stamina)
Popularity ยท Low
YouTube
Searching YouTube...
Lyrics
Hivi Ama vile,huku ama kule
Shangwe nyingi ziko wapi roma huku ama kule,
Zinanichanganya sijui ni huku ama kule,
Maana ninazoskia huku ndio ninazo ziskia kule,
Hivi Ama vile,huku ama kule
Shangwe nyingi ziko wapi roma huku ama kule,
Zinanichanganya sijui ni huku ama kule,
Maana ninazoskia huku ndio ninazo ziskia kule
Mimi nampenda uncle Magu mwokozi wa makapuku.
Ah mimi ukinikata damu yangu ni lowasa mtupu,
So wanangu wa ukawa vidole viwili juu,
Hapa kazi tu ikulu mtapasikia tu,
Hata nifungwe mimi ni Arsenal sio Man U,
Hamna lolote ndio maana hamchezi UEFA msimu huu,
Bongo mimi ni Yanga tena vikombe ni tele,
Ah wapi wanangu wa simba piga kelele,
Ah nampenda snura ana bonge la chura,
Mh mm.nampenda shishi mwanamke sura,
Ah acha ubishi dogo,
Acha ligi,mimi amber lulu ndio mkali,
Mimi Gigy,
Eti mziki una team haya team kiba mko wapi,
Team hazijengi hata wasafi wakijenga masaki,
Mimi wema we boya tu unalipi la kusema?,
Mimi zari niko zangu madale na naishi vyema
Hivi Ama vile,huku ama kule
Shangwe nyingi ziko wapi roma huku ama kule,
Zinanichanganya sijui ni huku ama kule,
Maana ninazoskia huku ndio ninazo ziskia kule,
Hivi Ama vile,huku ama kule
Shangwe nyingi ziko wapi roma huku ama kule,
Zinanichanganya sijui ni huku ama kule,
Maana ninazoskia huku ndio ninazo ziskia kule
Mimi mziki ukinishinda mdogo wangu nitakuwa mkulima,
Mimi nitakuwa mfugaji nifuge vyote vya nchi nzima,
Lakini kweli nikila ugali si nitahitaji na nyama?,
Basi bifu la wakulima na wafugaji halina maana,
Ila Ronaldo mkali ki-soccer hana mpinzani,
Hawezi kumzidi Messi wakikutana Dimbani,
Kwanza Madrid siwapendi washanichania mikeka,
Acha soccer huliwezi ka-bet kwenye mieleka,
Hivi Ney na Madee nani raisi wa manzese,
Hata udiwani hawafai,kwanza mmoja ana kithethe,
Nisha zunguka nchi nzima kila kona ninashabiki,
Acha uwongo hivi ushafanya show kibiti,
Madereva tunaleseni makonda mnatupa loss,
Mbona makonda hatuna vyeti ila tunaaminiwa na boss,
Ila wewe bwege ukimuacha mama Ivan utapata dhambi,
Walahi! nishaweka kambi ninampenda Mange Kimambi
Hivi Ama vile,huku ama kule
Shangwe nyingi ziko wapi roma huku ama kule,
Zinanichanganya sijui ni huku ama kule,
Maana ninazoskia huku ndio ninazo ziskia kule,
Hivi Ama vile,huku ama kule
Shangwe nyingi ziko wapi roma huku ama kule,
Zinanichanganya sijui ni huku ama kule,
Maana ninazoskia huku ndio ninazo ziskia kule
Hehehee.Ila mdogo wangu wewe unapenda sana Ligi wewe,
Yani wewe unaweza ukabisha mpaka outro wewe,
Kwa mfano mimi kama mimi yani,
Mimi nakumbia namkubali Mussa babas wa babas,
Wai... kimpango wako bwana wewe,
Si unajua watu wafupi wabishi, afu si unajua tabaka la morogoro,
Mimi namkubali chief Kiumbe wewee,
Hahaa