Skip to content
Lyric
Dive
Public playlists
My playlists
Search
Sign in
SMS
Barnaba
Popularity ยท Low
+
๐ฐ๐ช Swahili ยท Original
0
0
YouTube
Searching YouTube...
Lyrics
Original
Translation
Bilingual
Siijui hii SMS baby
Una haki, sikulaumu na una kila sababu
Kuni-command kuniuliza, "Huyu ni nani?"
Siku-command mume wangu, ila nalinda pendo langu
Upo ndani ya himaya yangu ndo maana nina hofu na zao langu
Uko sahihi ila inabidi uchunguze kwanza
Ukipata jibu ndo u-panic sio, "Pu" tu unavimba
Hayo si maneno mume wangu, kuyanena mbele yangu
Unazipelekea hisia zangu, kuhisi naibiwa zao langu
Mmh, basi baby nakupa message usome
Na ukishasoma usilalamike
Usini-set mume wangu, nataka kuipooza roho yangu
Suluhisho la moyo wangu, mpigie upooze mtima wangu
Tusigombane kisa message hiyo, baby siijui
Amekosea namba, haipaswi kulalamika
Haiwezekani tumpigie, 'weke loudspeaker tumsikie
Haiwezekani akosee namba, wakati wenye simu ni wengi
Tusigombane kisa message hiyo, baby siijui
Amekosea namba, haipaswi kulalamika
Haiwezekani tumpigie, 'weke loudspeaker tumsikie
Haiwezekani akosee namba, wakati wenye simu ni wengi
ย
Chozi langu thamani lanitoka chumbani, eh
Namlilia nani kama si' wewe
Najua ni hasira, zikipoa mpendwa utaelewa
Hata maji ya moto hupoa mapema yakipepewa
Usinipoteze lengo mume wangu
Unataka kuzifumba mboni zangu
Mpigie huyo mwenzangu
Ili nijue siko peke yangu
Haya kachukue charger yangu
Ipo kwenye mkoba wangu
Ukisharudi tena kwangu
We utafurahi mke wangu
Tusigombane kisa message hiyo, baby siijui
Amekosea namba, haipaswi kulalamika
Haiwezekani tumpigie, 'weke loudspeaker tumsikie
Haiwezekani akosee namba, wakati wenye simu ni wengi
Wooh! Ona sasa, zimefutika namba
Zimefutika sms kwenye inbox
Aah, bwana baba umezifuta makusudi
Mbona mi mwanzo niliziona kwa macho yangu
Tusigombane kisa message hiyo, baby siijui
Amekosea namba, haipaswi kulalamika
Haiwezekani tumpigie, 'weke loudspeaker tumsikie
Haiwezekani akosee namba, wakati wenye simu ni wengi
Haiwezekani tumpigie (sina namba)
'Weke loudspeaker tumsikie (si unajua zimefutika)
Haiwezekani akosee namba, wakati wenye simu ni wengi
Achana nayo
Mm! Haya bhana
ย