Skip to content
Lyric
Dive
Public playlists
My playlists
Search
Sign in
Mariana
Eric Wainaina
Popularity ยท Low
+
๐ฐ๐ช Swahili ยท Original
0
0
YouTube
Searching YouTube...
Lyrics
Original
Translation
Bilingual
Mariana, Mariana
Nimechoka kusota
Nimeamua leo ni leo
Nitabadili picha
Mariana, Mariana
Niliomba unipe mwaka
Usitupe upendo wetu
Na usiamke kutoka ndoto yetu
Nilinunua baiskeli
Kupitia mkopo wa benki
Kusafirisha abiria
Lakini iliibiwa
Mariana, Mariana
Ulitafuta visa
Ya nchi ya Uropa
Utaniacha juu ya pesa
Hakuna atakayeweza
Kukupenda vile nakupenda
Najua upendo hauliwi
Lakini moyo haudanganywi
Nilinunua shamba
Na nilipanda mimea
Ya kuuza Marikiti
Lakini ukame ukanirudisha magotini
Mariana, Mariana
Nilikuwa nimechoka
Kwa vile umaskini
Utafanya unitoroke
Mariana, Mariana
Nilikomboa bunduki
Niliamua leo ni leo
Nilikuwa na mpango mufti
Kama vile kwenye movie
Niliingia kwa benki
Nilisema lala chini
Nikajaziwa tikiti (oooooh)
Basi mimi ni huyo
(Basi mimi ni huyo)
Nikajivuta upesi
(Nikajivuta upesi)
Nikauficha mzigo
(Nikauficha mzigo)
Na nimeiba gari
(Nimeiba gari)
Naenda mwendo kasi
(Naenda mwendo kasi)
Lakini kasi haishindi risasi
(Ooh ooh)
Zinanyesha kama mvua
(Zinanyesha kama mvua)
Naomba Mungu atanipokea
(Ooh ooh)
Ooh oooh
Ukiulizwa kwa nini
Kwa makumbusho yangu
Waeleze nilikataa kuishi
Na matumaini pekee
Mariana, Mariana
Jambo la mwisho
Kwa mizizi ya mti wetu
Nimekuachia zawadi
Ili usinitoroke
ย