Skip to content
Lyric
Dive
Public playlists
My playlists
Search
Sign in
Mtazamo
Afande Sele feat. Solo Thang & Professor Jay
Popularity ยท Low
+
๐ฐ๐ช Swahili ยท Original
0
0
YouTube
Searching YouTube...
Lyrics
Original
Translation
Bilingual
1.
Yo yo Hakuna S bila O, L bila O mwingine aitwe Thang bila Solo
Shupavu awajibike kama Apollo
Jay, afande ni ukuta wa vichochoro
Yo nadhani nadhani ni mtazamo wa fani Ile dhana ni uhuni wameleta hawa katuni
kuna ku rap na kubwata marepa na ma-rapper
Katuni tungo tata wapi ulipo wewe kaka
Unakuwa mtumwa ili upewe promo kuuza
Au kama ni demu ukalale kwa producer
Mapromota wanauma tu na hawajui kupuliza na siku wakipuliza ujue kidonda kishaoza
Natamani kuwa huru mnyonyaji asinidhuru wanaitwa ma-mc hawajui mitindo huru
Huu mtazamo wangu naona vingi vioja
Yaani watangazaji ndio ma-manager
Vidato 6 nilivyopitia ndivyo vinavyonisaidia mbunifu ukizingatia hata wakinibania ni kipaji tu ni mtazamo tu msikasirike washkaji haya mawazo tu
ร2
Ni mtazamo zamo Mc usiogope kivuli bora ukemee mabaya na usifie mazuri
Ni mtazamo zamo Mc usikwepe umande
Okoa Sanaa ya Bongo ili uchumi upande
Ni mtazamo zamo Mc usiogope kivuli bora ukemee mabaya na usifie mazuri
Ni mtazamo zamo Mc usikwepe umande mi mi Ulamaa, professor Jay Afande
2.
Ni mtazamo rap inakuwa ni mikingamo sasa watoto wadogo wanajiita watu wa makamo wanakwenda hatua 10 wanarudi 2 wanajipongeza bila kuzingatia hatua 8 walizopoteza Hawa ni mafukara wa akili zao na uwezo wao wasiotambua nini na nini ni hatima yao magwiji vichwa chini nadhani wanatunga sheria lakini sheria msumeno isije ikawarudia
Yes ma-underground wanafanya rap inang'ara lazima muwe vinara imara kwenye msafara, rap na mazingaombwe abadani haviendani musitegemee tawire ikuokoe katika fani
Ni vema ukafikiri kabla ya kufanya maamuzi Tazama mbele usije ukanywa chai kwa mluzi naamini askari shupavu ni lazima upitie depo vinginevyo ndugu yangu utakuwa unapaka rangi upepo
Kama unapata 1 iweje usipate na 100 hiyo inawezekana kwa wote mlio na nia sioni sababu ya msingi kuomba kwenye mitaa kama una kipaji iweje ufe na njaa
Repeat ร2
3.
Asante professor Jay, Majani na Ulamaa mmegusa ninapopataka
Nami kwenye mtazamo nina jambo nataka kuweka
Maana kila kukicha Mcs' wanaongezeka nasema very nice, yes rap kama dhehebu
Mcs' kama wafuasi wingi wa wasanii inaonesha ni dini safi yaani imekubalika
Waumini tupo wengi lakini bado nina shaka sijapata uhakika wote tumesadiki au wengine ni feki mmetumwa kama mamluki maana yake hamna maana mnavyorap mistari imekosa vina, yenye vina haina maana na kila mnapokaa mnapenda kusengenyana mnapenda kutetana na mnapenda kulumbana
Mimi naogopa sana kwa jinsi ninavyoelewa mwishoni mtatukanana ama inawezekana mwishoni mkaja chinjana na wote tunaorap tuonekane hatuna maana, wapi ilipo taarabu ilikuja kwa kishindo hata wagumu walishahusudu kwa ajili ya malumbano mwishoni ikafa kibudu, shabiki piga simu changia mawazo yako ni nani tutamlaumu kama rap itasizi kwa kuendekeza upuuzi
Nani tumchune ngozi producer aliyerekodi ama lover Dj anaepiga kwenye kipindi
Wengi wanapenda rap ajabu rap haiwapendi, waungwana wanaiacha wapumbavu Hawaambiliki hivi kwani lazima tuwe wote wanamuziki mimi nadhani ingetosha wengine mbaki ushabiki huu ni wangu mtazamo masela msijenge chuki (hata na Majani)
Repeat ร2
ย