Skip to content

Nisamehe (Omba Msamaha)

Bony Mwaitege
Popularity ยท Low

YouTube

Searching YouTube...

Lyrics

Lina faida zake Hili neno lisome Ndugu yangu litumie Nisamehe, baba nisamehe (Mwanao naomba) Nisamehe baba, naomba nisamehe bure (Mwana mpotevu alisema) Nisamehe, baba nisamehe (Nisamehe baba) Nisamehe baba, naomba nisamehe bure Nimeyatambua makosa yangu Baba Nisamehe, baba nisamehe (Nisamehe Baba) Nisamehe baba, naomba nisamehe bure(Baba) Nisamehe, baba nisamehe (Mwana mpotevu alisema) Nisamehe baba, naomba nisamehe bure eeh Paliukua na baba mmoja Aliyekuwaga na wana wawili Yule mdogo alimwambia baba yake Nipe baba sehemu yangu ya mali Alipopewa akaenda nchi ya mbali Akatumia pesa zote kwa anasa Alipoishiwa pesa alipata shida Akadiriki kula na nguruwe Akawaza ndani ya moyo wake "Kwa nini mimi nipate shida?" Watumishi wanagapi wako kwa baba Wanakula chakula na kusaza Akaamua arudi kwa baba yake Ili aombe msamaha Akaamua arudi kwa baba yake Ili aombe msamaha Nisamahe akasema nisamehe baba Nimekosa naomba nisamehe Nisamahe akasema nisamehe baba Nimekosa naomba nisamehe bure Nisamehe, baba nisamehe (baba Wewe) Nisamehe baba, naomba nisamehe bure (Mwana mpotevu alisema) Nisamehe, baba nisamehe Nisamehe baba Naomba nisamehe bure eeeh Kuna watu wanashindwa kuishi na watu Sababu hawawezi kuomba msamaha Kuomba msamaha wanadhani ujinga Kuomba msamaha kumbe jambo la hekima Ndugu yangu jifunze kusema nisamehe Ukikosa, omba msamaha Kuomba msamaha wanadhani ujinga Kuomba msamaha kumbe jambo la hekima, nisamehe Nisamehe, baba nisamehe (Nisamehe) Nisamehe baba, naomba nisamehe bure (Nisamehe) Nisamehe, baba nisamehe (Nisamehe) Nisamehe baba, naomba nisamehe bure eeeh Unaweza poteza bahati yako bure Kwa kushindwa kuomba msamaha Unaweza kumpoteza mume au mke Kwa kushindwa kuomba msamaha Unaweza kumpoteza mchumba wako mpendwa Kwa kushindwa kuomba msamaha Unaweza kudhani una mikosi kumbe huna Tatizo lako huombi msamaha Ndugu yangu jifunze kusema, nisamehe Vinginevyo utapoteza ajira yako Ndugu yangu jifunze kusema, nisamehe Penginevyo unaweza ukapoteza bahati yako Nisamehe, baba nisamehe (Naomba nisamehe) Nisamehe baba, naomba nisamehe bure (Mwana mpotevu alisema) Nisamehe, baba nisamehe (Nisamehe baba) Nisamehe baba, naomba nisamehe bure Nimetambua makosa yangu jamani Nisamehe, baba nisamehe (Naomba nisamehe) Nisamehe baba, naomba nisamehe bure (Mwana mpotevu alisema) Nisamehe, baba nisamehe (Nisamehe baba) Nisamehe baba, naomba nisamehe bure Nikisoma maandiko najifunza Kuomba msamaha ni jambo la hekima Mfalme Daudi alipogundua Amemkosea Mungu, aliomba msamaha Alitubu tena kwa machozi Akasema eeh Mungu wangu nisamehe Mtume Petro alipogundua pia Amemkana Yesu, aliomba msamaha Alitubu tena kwa machozi Akasema eeh Mungu wangu nisamehe Wewe na mimi ni nani ata tushindwe Kujishusha na kuomba msamaha Wewe na mimi ni nani ata tushindwe Kujishusha na kuomba msamaha, tusamehewe Nisamehe, baba nisamehe (Samehewe) Nisamehe baba, naomba nisamehe bure (Halleluhya, nisamehewe) Nisamehe, baba nisamehe (Nisamehe baba) Nisamehe baba, naomba nisamehe bure Umeyatambua makosa yako, tubu ndugu yangu Nisamehe, baba nisamehe (Samehewe) Nyosha mikono Nisamehe baba Mbele ya Mungu wako Naomba nisamehe bure Sema na tubu leo Nisamehe, baba nisamehe (Nisamehewe dhambi zangu zote) Nisamehe baba, naomba nisamehe bure (Mungu akutakase kwa jina la Yesu) Usamehewe, samehewe Usamehewe, samehewe Mungu anapenda wanaotubu Anayetubu anasamehewa bure Nisamehe (bure) Baba nisamehe (Samehewe) Nisamehe baba, naomba nisamehe bure (nisamehewe sema nisamehe Nisamehe, baba nisamehe (mwana mpotevu aliomba Msamaha) Nisamehe baba, naomba nisamehe bure Nisamehe, baba nisamehe (Ndugu yangu tubu) Nisamehe baba (usamehewe) Naomba nisamehe bure (Kama mwana mpotevu) Nisamehe, baba nisamehe (aliomba msamaha, akasamehewa) Nisamehe baba, naomba nisamehe bure (akasamehewa) Nawe ukitubu akasamehewa