Skip to content

Pastor

Roma
Popularity ยท Low

Listen

YouTube

0:00 / 0:00
Loading YouTube player...
Lyrics offset
Synced

Lyrics

Yeah Wacheni watoto wadogo waje kwangu Mana ufalme wa mbinguni ni wao J.rider where you are Am the pastor of this church Am the pastor of this church Am the... its tongwe records Fanya ishara ya msalaba Upokee haya mahubiri Mimi ni mteule, nina waletea injili Nina ushuhuda wa kiroho Bwana yuwa je msubiri Natangaza upako, na habari za mnara wa babeli Wachungaji wanalumbana wakigombania waumini, wanalala Wakiamka wanaanzisha dini Hawaogopi damu ya msalaba Bible wanaifanya biashara we sio yesu Hatakama baba yako fundi seremala We ni nani usokosea kila unayemuombea anapona Hatutaki shuda za uongo Aminini nyote mtachomwa Ndani ya vazi la suti unakebehi Wakatoliki Mtaleta dini zote ila R.C itabaki Hata kristo alipoponya hakutaka malipo Account yako imejaa sadaka zetu Wakristo Toba yako haijaswihi halafu unajiita una Upako So kila atakayenita bwana basi ataiyona pepo We nina unayejiita nabii kwenye jamii Hizi nyakati za mwiลŸo soon atashuka masih Piga magoti tuswali ameen Piga magoti tuswali (ameen) Waumini wamekimbia kanisa Madhehebu yanaongezeka Hizi nyakati za mwisho Check manabii wa uongo mwana wa adam ni waja (ameen) Mwana wa adam ni waja(ameen) 2... Laiti ningewezaaa ningekugeuza jiwe la chumvi Vipi unipangie sadaka pastor gani We mlanguzi Hakika ili neno listumikie mabwana wa2 Siasa na kanisa kama hadisi za cain na abel Ka sabato wasokula kitimoto wala kambare wanasadiki mbele ya haki Wanaamini agano la kale Mnatangaza ufahari wenu kwenye vikapu cha sadaka Hakuna sadaka ya kweli kama kumchinja isack Kanisa lako halifanani na ufalme wa jehova Madhehebu yanajitenga kama makundi ya bongo fleva Heshima ya mkatoliki inashuka kama theluji Dini mmeifanya miradi kwa kivuli cha uchungaji Kanisani mnaonyeshana ufahali wa kuvaa bazeee Hekalu mnalichafua Kwa sadaka ya pedeshee Biblia hujaimaliza unataka uzima wa milele Usije ukatuchoma moto Ka wafuasi wa kibwetele (Chorus). We nina unayejiita nabii kwenye jamii Hizi nyakati za mwiลŸo soon atashuka masih Piga magoti tuswali ameen Piga magoti tuswali (ameen) Waumini wamekimbia kanisa Madhehebu yanaongezeka Hizi nyakati za mwisho Check manabii wa uongo mwana wa adam ni waja (ameen) Mwana wa adam ni waja(ameen) Hizi nyakati za mwisho soon atashuka masih Wewe una mamlaka gani mpaka unajiita nabii Kukataza waumini wasivae mapambo Kwa kujaji ili pesa wakupe sadaka Na kisha unafanya mtaji We m hungaji umekusanya waumini Kwenye vijiji Ukawaongoza sala ya toba Kama yohanna mbatizaji Unabeba gunia la zambi Na yesu kumvika taji Usiniekee mkono kichwani huna katamu ya uponaji Imani yako ndogo kama punje ya radani Uza mali zako zote pesa uwape maskini Si unatupa kiini macho unatumia gari ya kanisa Halellujah halellujah kumbe unatuibia sadaka Yesu hakuwa mganga wa kienyeji Japo alimponya kipofu kwa tope la mate yake Ila kwako napata hofu Ehhh mungu napiga goti hiki kikombe kiniepuke mwana wa adamu ni waja basi tungoje ashuke (Chorus). We nina unayejiita nabii kwenye jamii Hizi nyakati za mwiลŸo soon atashuka masih Piga magoti tuswali ameen Piga magoti tuswali (ameen) Waumini wamekimbia kanisa Madhehebu yanaongezeka Hizi nyakati za mwisho Check manabii wa uongo mwana wa adam ni waja (ameen) Mwana wa adam ni waja(ameen) Angalieni mtu asiwadanganye Mana wengi watakuja kwa jina langu wakisema. mimi ni christo Nao watadanganya wengi(halellujah) Emeeen . Manabii wengi wa uwongo watatokea Kutakuwa na dhiki kubwa siku hiyo Je hamsadiki ya kuwa hizi ni ishara kwamba mwana wa adam ni waja Emeeen . Basi hakikisheni mkiswali mana hamjui saa wala siku I am the pastor of this church I am the pastor of this church I am the... Its tongwe records...