Skip to content
Lyric
Dive
Public playlists
My playlists
Search
Sign in
Siku za Kilio Zimepita
Ambassadors of Christ Choir
Popularity ยท Low
+
๐ฐ๐ช Swahili ยท Original
0
0
Listen
YouTube
1
2
3
0:00 / 0:00
Loading YouTube player...
Lyrics offset
Synced
Lyrics
Original
Translation
Bilingual
Sauti ilisikika mjini Rama, kilio na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake, lakini hakutaka kufarijiwa kwa kuwa hawako tena.
Bwana asema hebu zuia sauti yako usilie mama, na macho yako kamwe yasitoke machozi tulia ee jipe moyo ร2
ย
Maana kazi yako itapata thawabu na kwa nguvu mpyaร2 utainuliwa tena.
Wakati tulio nao, si wa kuomboleza tena, siku za kilio zimepita zimekwisha, aanha.
Sasa twasonga tena mbele kwa kazi yake bwana matokeo kwamwe hayatatukatisha tamaa, anhaa.
Na tutaweza yote, kwa jina lake mwenye nguvu, na kwa mkono wake yeye mwenyewe atatuongozaร2
ย
Twatiwa nguvu kwa neno lake bwana Mungu, uuhuu, asemapo baada hayo yote nitarejea, nami nitaijenga tena nyumba yake Daudi iliyoanguka nitajenga tena maanguko yake nitaisimamisha,
Kwa ajili yake bwana twaweza kuuwawa mchana usiku kucha twahesabiwa kuwa kama kondoo wasubirio kuchinjwa,
Lakini katika mambo haya yote tumeshinda na zaidi ya kushinda kwa yeye aliyetupenda jina lake lisifiwe milele.
Baada ya siku hizo za kupigwa vikali
Kama alivyoahidi nguvu mpya ametupatia tena.
Wakati tulio nao si wa kuomboleza tena siku za kilio zimepita zimekwisha anhaaa.
Sasa twasonga tena mbele kwa kazi yake bwana, matokeo kamwe hayatatukatisha tamaa, anhaaa.
Natutaweza yote kwa jina lake mwenye nguvu na kwa mkono wake yeye mwenyewe atatuongozaร3
ย
Kagera Tanzania
ย