Mapenzi Yananitatiza
Patricia Hillary
Popularity ยท Low
Listen
YouTube
0:00 / 0:00
Loading YouTube player...
Lyrics offset
Synced
Lyrics
Jamani mapenzi, yananitatiza, Kulala siwezi, kusema siwezi
Chakula sitaki, nakiiona sumu, Mapenzi yamenivaa, nami ugenini
Akili imenipaa,
hata njia siioni, Mapenzi
yana hadaa, ya kweli nawambieni
Haiba imepotea, uzuri umenitoka, mali imeangamia, maradhi hayakutoka,
Mwenzenu nimepotea,
muokozi kanitoka,
Enyi wenye ukarimu,
siri nawatobolea
Moyo umepata sumu,
madawa hayakufaa,
Kupenda kitu adimu, nawambia kuna baa
Ya kweli nawambieni, myatie akilini msipende ugenini, mtaingia hatiani
Mtalala majiani, wazimu tele vichwani